Siri ya Jina la Mwezi wa Muharram, Maana za Miezi 12 ya Kiislamu na Wajibu wa Muumini

Sifa zote njema zinamstahiki Allah (Subhanahu wa Ta'ala), Mola wa walimwengu wote, aliyekadiria nyakati na akajaalia miezi kuwa kipimo cha ibada na maisha ya mwanadamu. Swala na salamu zimfikie mwalimu wa ummah, Mtume Muhammad (Swallah Llahu 'alayhi wa sallam), kizazi chake na maswahaba zake waliotunza misingi ya dini hii kwa uaminifu mkubwa. Kila mfumo thabiti wa maisha kuna alama zake za utambulisho, na katika Uislamu, Kalenda ya Hijriyah ndio dira yetu kuu ya nyakati. Hata hivyo, Waislamu wengi wamezoea kutumia majina ya miezi hii bila kufahamu chimbuko lake, maana zake, na wajibu uliopo ndani ya kila mwezi. Kupitia makala hii kabambe kutoka jukwaa lenu la AMAN VISSION , tutazama kwa undani kuelewa siri iliyopo nyuma ya jina la mwezi wa Muharram , maana za miezi yote 12, na mambo anayotakiwa kuyatekeleza Muumini katika kila kituo cha mzunguko wa mwaka. Siri ya Jina Muharram: Je, Lilitokana na Tukio Gani? Neno "Muharram" (المحرّم) kihisaba...

Elimu na Mafunzo ya Dini ya Kiislamu Yanayosimamiwa na Mfumo wa AMAN VISSION: Fursa ya Kujifunza kwa Ngazi Zote za Tamhiid, Mutawassitwah, na Thaanawiy

Katika safari ya kuelekea ujenzi wa jamii iliyonyooka, elimu ndio taa inayomulika njia na kuondoa giza la ujinga. Hata hivyo, ili elimu ilete athari chanya na matunda yanayoonekana, ni lazima iendeshwe kwa nidhamu, mpangilio, na mfumo thabiti unaomfanya mtafutaji wa maarifa ajue wapi anapoanzia na wapi anapoelekea. Elimu isiyo na mtaala maalum mara nyingi huacha maswali mengi kuliko majibu katika akili ya mwanafunzi.

Kupitia mfumo wa AMAN VISSION, unaoendeshwa chini ya usimamizi wangu wa karibu, tumeweka kipaumbele kikubwa kwenye ufundishaji wenye dira na malengo. Ili kufikia azma hii, tunafurahi kuwasilisha kwenu Silabasi Kamili ya AMAN VISSION. Huu ni mtaala rasmi na wa kina wa masomo ya Elimu ya Dini ya Kiislamu na Lugha ya Kiarabu uliogawanywa katika ngazi kuu tatu za kitaaluma, kwa mujibu wa Qur'aan Tukufu na Sunnah za Mtume wetu Muhammad (S.A.W).

Silabasi hii imeandaliwa kwa kuzingatia vitabu teule na vya asili vilivyotungwa na wanachuoni wakubwa na wajuzi wa ummah huu. Masomo haya yanatolewa kwa njia mbili: Online (kwa njia ya mtandao) na Darasa la ana kwa ana, yakigawanywa katika hatua zifuatazo:


Ngazi ya Kwanza: Tamhiid (Msingi Mkuu / Utangulizi)

Hii ni ngazi ya awali inayochukua Muda wa Mwaka 1 (Mihula Miwili / Semesters 2). Imetengenezwa maalum kwa ajili ya kuweka msingi thabiti wa kiimani, kiibada, na kilugha kwa wanaoanza safari yao ya kielimu (Beginners). Masomo na vitabu vinavyofundishwa katika ngazi hii ni:

  • 1. Qur'aan na Tajwiid: Kusoma kitabu cha Al-Qaaidat Nnooraaniyyah kwa ajili ya kutambua herufi na kupata matamshi sahihi ya maneno, kikifuatiwa na kitabu cha Tuhfatul Atwfaal ili kujenga misingi ya Tajwiid ikiwemo sheria za Nun Sakina na Tanween.
  • 2. Hadiith na Sunnah: Kusoma na kuhifadhi kitabu cha Al-Arba'iina Nnawawiyyah kuanzia Hadiithi ya 1 hadi ya 20, inayofundisha misingi ya mwanzo ya dini na nia njema.
  • 3. Fiqhi na Al-Usuul: Kujifunza misingi ya ibada za kila siku kupitia kitabu cha Al-Fiqhul Muyassar (Sehemu ya Twahara na Swala).
  • 4. Aqiidah na Tawhiid: Kumjua kwa usahihi Mola Muumba, Mtume wake, na dini kupitia kitabu muhimu cha Thalaathatul Usool (Misingi Mitatu).
  • 5. Taariikh na Siirah: Kujifunza wasifu na maisha ya Mtume (S.A.W) kipindi cha Makka kupitia Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 1).
  • 6. Lugha ya Kiarabu: Kujenga misingi ya mazungumzo na herufi kupitia Duruus LLughatul Arabiyyah (Kitabu cha 1) pamoja na kujifunza uandishi sahihi kupitia Qawaaidul Imlaa.
  • 7. Adyaan na Maadili: Kuweka misingi ya tabia njema na akhlaq kupitia kitabu cha Riyaadh Sswaaliheen (Mlango wa Adabu).

Ngazi ya Pili: Mutawassitwah (Ngazi ya Kati / Uchambuzi)

Baada ya kufuzu ngazi ya kwanza, mwanafunzi anavuka kwenda ngazi ya kati inayochukua Muda wa Mwaka 1 (Mihula Miwili / Semesters 2). Hapa elimu inaanza kupanuka na mwanafunzi anajengewa uwezo wa kuchambua masuala ya kisheria na kilugha kupitia masomo yafuatayo:

  • 1. Qur'aan na Tajwiid: Kujifunza sheria kamili na za kina za Tajwiid kwa njia rahisi ya mifano kupitia kitabu cha Hidaayatul Mustafiid (kwa maswali na majibu).
  • 2. Hadiith na Sunnah: Kukamilisha hadithi zilizobaki katika kitabu cha Al-Arba'iina Nnawawiyyah (Hadithi ya 21 hadi 42).
  • 3. Fiqhi na Al-Usuul: Kusoma fiqhi ya kina ya ibada na muamalat kupitia Matnul Ghaayat Wattaqriib (Abi Shujaa'h) na kupata utangulizi wa misingi ya Fiqhi kupitia kitabu cha Al-Waraqat cha Imam Al-Juwayni.
  • 4. Aqiidah na Tawhiid: Kujifunza namna ya kulinda itikadi na kuepuka ushirikina kupitia vitabu vya Al-Qawa'idul Arba'ah (Kanuni Nne) na ufafanuzi wa tauhidi ya ibada kupitia Kitabu Ttawheed.
  • 5. Taariikh na Siirah: Kuendelea na historia ya ujenzi wa dola ya Kiislamu ya Madina na zama za makhalifa kupitia Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 2 na 3).
  • 6. Lugha ya Kiarabu: Kukuza sarufi na mnyambuliko wa lugha kupitia Duruus LLughatul Arabiyyah (Kitabu cha 2 & 3), misingi ya Nahwu kupitia Al-Ajruumiyyah, na Swarfu kupitia Matnul Binaa wal-Asaas.
  • 7. Adyaan na Maadili: Kujifunza mambo ya kuepuka kupitia Kitaabul Kabaair (Madhambi Makubwa) na mbinu za mwanzo za ulinganizi kupitia Adda'wah ila Llaah.
"Mtaala huu umenyooka na kuratibiwa kwa namna ambayo inamtoa mwanafunzi kwenye hatua ya ugeni wa lugha na misingi, na kumfikisha kwenye daraja la ukomavu kamili wa kielimu na kimaadili."

Ngazi ya Tatu: Thaanawiy (Ngazi ya Juu / Uborezaji)

Huu ndio kilele cha sasa cha mfumo wa AMAN VISSION. Ngazi hii inachukua Muda wa Mwaka 1 (Mihula Miwili / Semesters 2) na imetengenezwa kwa ajili ya kuwanoa wale wanaotaka kuwa walimu, viongozi, na wasambazaji wa heri katika jamii kupitia uchambuzi wa juu:

  • 1. Qur'aan na Tajwiid: Kusoma sifa za ndani na matamshi ya kina ya herufi za Qur'an kupitia matni maarufu ya Matnul Jazariyyah.
  • 2. Hadiith na Sunnah: Uchambuzi wa hadithi za kisheria na hukumu moja kwa moja kutoka kwenye vyanzo vikuu vya Umdatul Ahkaam na Buluughul Maraam.
  • 3. Fiqhi na Al-Usuul: Kusoma fiqhi pana, ya kielimu na isiyofungamana na ushabiki wa kimadhehebu kupitia kitabu cha Manhaj Ssaalikiin.
  • 4. Aqiidah na Tawhiid: Kusimama kwenye itikadi sahihi isiyo na mapungufu juu ya Majina na Sifa tukufu za Allah kupitia kitabu cha Al-Aqiidatul Waaswitwiyyah.
  • 5. Taariikh na Siirah: Kusoma wasifu wa kina kabisa wa maisha ya Mtume (S.A.W) kupitia Ar-Raheequl Makhtoom na historia ya Mitume waliotangulia kupitia Qiswasul Anbiyaai cha Ibn Kathiir.
  • 6. Lugha ya Kiarabu: Kujifunza kusoma kwa ufasaha, msamiati, insha, na usemi kupitia Al-Qiraa'at Rrashiidah (Taabiir & Kitaabah) pamoja na uandishi wa juu kupitia Khattw na Imla.
  • 7. Adyaan na Maadili: Kuelewa makundi, madhehebu, na kulinganisha dini kupitia kitabu cha Al-Milal wa Nnihal, sambamba na kujifunza misingi mikuu ya Da'wah na maadili ya uongozi.

Hitimisho na Wito wa Kujiunga

Silabasi hii ni ushahidi tosha kwamba elimu inayotolewa ndani ya AMAN VISSION sio ya kubahatisha, bali ni mfumo uliopangwa kitaaluma ili kukupa wewe au mtoto wako maarifa sahihi yatakayomfaa duniani na akhera. Milango ya usajili ipo wazi kwa ajili ya ngazi zote tatu.

Tunawakaribisha wote kuja kujiandikisha na kuanza safari hii yenye baraka kubwa. Kuwa sehemu ya familia yetu leo, uanze kujifunza dini yako kwa nidhamu, wepesi, na kwa usahihi wa hali ya juu.

Comments