MITAALA YA MASOMO YA KIISLAMU
Academic Curriculum & Training Levels
Mfumo wa elimu wa AMAN VISSION umeundwa kwa umakini mkubwa ili kutoa mafunzo ya kina na sahihi ya Dini ya Kiislamu. Maudhui yetu yanalenga kujenga jamii yenye imani thabiti, elimu ya kutosha, na tabia njema kwa mujibu vya Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur'an Tukufu) na Sunnah za Mtume Muhammad (S.A.W) kupitia ngazi kuu tatu za kitaaluma ambazo kila moja inachukua muda wa mwaka mmoja.
Ngazi Kuu za Mtaala Wetu
Ngazi ya Kwanza: TAMHIID (Utangulizi)
Muda: Mwaka 1 (Semesters 2)
Lengo la Elimu: Huu ni msingi mkuu wa kumuandaa mwanafunzi katika kusoma maneno ya Allah kwa usahihi na kujenga misingi ya mwanzo ya nidhamu na itikadi.
- Qur'aan na Tajwiid: Al-Qaaidat Nnooraaniyyah (herufi na matamshi) na Tuhfatul Atwfaal (misingi ya Tajwiid).
- Hadiith na Sunnah: Al-Arba'iina Nnawawiyyah (Hadithi ya 1 - 20).
- Fiqhi na Al-Usuul: Al-Fiqhul Muyassar (sehemu ya Twahara na Swala).
- Aqiidah na Tawhiid: Thalaathatul Usool (Kumjua Mola, Mtume, na Dini).
- Taariikh na Siirah: Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 1 - Kipindi cha Makka).
- Lugha ya Kiarabu: Duruus LLughatul Arabiyyah (Kitabu cha 1) na Qawaaidul Imlaa (misingi ya uandishi).
- Maadili na Da'awah: Riyaadh Sswaaliheen (Mada zilizoteuliwa za Akhlaq na adabu).
Ngazi ya Pili: MUTAWASSITWAH (Kati)
Muda: Mwaka 1 (Semesters 2)
Lengo la Elimu: Kumvusha mwanafunzi kuelekea kiwango cha uchambuzi wa lugha ya Kiarabu, misingi ya Fiqhi, na kulinda usalama wa kiitikadi.
- Qur'aan na Tajwiid: Hidaayatul Mustafiid (sheria za usomaji kwa mfumo wa maswali na majibu).
- Hadiith na Sunnah: Al-Arba'iina Nnawawiyyah (Kukamilisha Hadithi ya 21 - 42).
- Fiqhi na Al-Usuul: Matnul Ghaayat Wattaqriib (Kitabu cha Abi Shujaa'h) na Al-Waraqat (misingi ya Fiqhi).
- Aqiidah na Tawhiid: Al-Qawa'idul Arba‘ah na Kitab at-Tawheed (ufafanuzi thabiti wa tauhidi na kuepuka shirki).
- Taariikh na Siirah: Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 2 & 3 - Kipindi cha Madina na Khilafa).
- Lugha ya Kiarabu: Duruus LLughatul Arabiyyah (Kitabu cha 2 & 3), Al-Ajruumiyyah (Nahwu), na Matnul Binaa wal-Asaas (Swarfu).
- Maadili na Da'awah: Kitaabul Kabaair (kujua madambi makubwa) na Adda‘wah ila Llaah (mbinu za ulinganizi).
Ngazi ya Tatu: THAANAWIY (Juu)
Muda: Mwaka 1 (Semesters 2)
Lengo la Elimu: Kiwango cha juu kinacholenga kumuandaa mwanafunzi kuwa kiongozi bora wa jamii, mlinganizi (Da'ee), na mtaalamu wa hukumu za kisheria.
- Qur'aan na Tajwiid: Matnul Jazariyyah (ushairi wa kina wa sifa na matamshi ya herufi).
- Hadiith na Sunnah: Umdatul Ahkaam na Buluughul Maraam (Hadithi za hukumu za kisheria).
- Fiqhi na Al-Usuul: Manhaj Ssaalikiin (Fiqhi pana ya kielimu na kivitendo).
- Aqiidah na Tawhiid: Al-Aqiidatul Waaswitwiyyah (Itikadi sahihi ya Ahlus Sunnah wal Jama'ah).
- Taariikh na Siirah: Ar-Raheequl Makhtoom na Qiswasul Anbiyaai (wasifu wa Mtume na kisa cha Mitume).
- Lugha ya Kiarabu: Al-Qiraa'at Rrashiidah (Taabiir & Kitaabah) na Khattw pamoja na Imla ya Juu.
- Maadili na Da'awah: Al-Milal wa Nnihal (makundi na kulinganisha dini) na Misingi ya Da'wah & Uongozi wa Kijamii.
Uendeshaji wa Shule, Vyuo na Nidhamu
🏫 Mfumo wa Shule na Vyuo
Mtaala huu umesanifiwa kukidhi vigezo vya ufundishaji wa ana kwa ana katika Shule za Msingi, Sekondari, na Vyuo vya Kiislamu, pamoja na mfumo wa masomo ya jioni (Madrasa) na kambi maalum za likizo.
💻 Mfumo wa Mtandaoni (Online)
Kwa wanafunzi wa masafa marefu, mtaala huu unatolewa kupitia madarasa ya kidijitali, ambapo vipindi vinarekodiwa na kuwepo kwa majaribio ya kila wiki ili kupima uelewa na maendeleo ya mwanafunzi.
📜 Kanuni na Sheria za Nidhamu
Kila mwanafunzi aliye chini ya mfumo huu anapaswa kuzingatia mahudhurio ya vipindi kwa wakati (zaidi ya 85%), kuvaa mavazi ya kiheshima (Suna na Hijabu kamili), na kudhihirisha akhlaq njema ndani na nje ya taasisi.
📝 Tathmini na Mitihani
Ili kuvuka kutoka ngazi moja kwenda nyingine, mwanafunzi atafanya tathmini ya katikati ya muhula (Coursework) na mtihani mkuu wa mwisho wa muhula (Final Exams) wa nadharia na vitendo (kusoma na kuhifadhi).
Miongozo ya Juu ya Taaluma: Mitaala yote na vitabu vinavyotumika vinaratibiwa na kusimamiwa kikamilifu chini ya uongozi mkuu wa taasisi ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyonyooka na yenye manufaa.
Comments
Post a Comment
Karibu kutoa maoni yako. Tafadhali andika kwa heshima, maadili na lugha yenye kujenga jamii.