RATIBA, SILABASI NA ADA KAMILI
Complete Syllabus, Class Schedules & School Fees
Karibu kwenye mwongozo rasmi na mchanganuo kamili wa Syllabus (Mitaala), Ratiba za Vipindi, na Mfumo wa Ada kwa ajili ya wanafunzi wa Kutwa (Day), Kambi (Bweni), na wale wanaosoma Online (Mtandaoni) ndani ya AMAN VISSION.
1. Mchanganuo wa Ada kwa Kila Mfumo
| Kitengo cha Somo |
Mfumo wa Kutwa (Day) |
Mfumo wa Kambi (Bweni) |
Mfumo wa Online (Mtandaoni) |
| Qur'aan na Tajwiid | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 50,000 / Mwezi | Tsh 5,000 / Mwezi |
| Hadiith na Sunnah | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 45,000 / Mwezi | Tsh 5,000 / Mwezi |
| Fiqhi na Al Usuul | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 50,000 / Mwezi | Tsh 5,000 / Mwezi |
| Aqiidah na Tawhiid | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 45,000 / Mwezi | Tsh 5,000 / Mwezi |
| Taariikh na Siirah | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 50,000 / Mwezi | Tsh 5,000 / Mwezi |
| Lugha ya Kiarabu (Idara Zote) | Tsh 15,000 / Mwezi | Tsh 60,000 / Mwezi | Tsh 10,000 / Mwezi |
| Adyaan na Daawah | Tsh 10,000 / Mwezi | Tsh 50,000 / Mwezi | Tsh 10,000 / Mwezi |
2. Ratiba za Masomo (Wiki, Mwezi & Mwaka)
A. Ratiba ya Kila Wiki (Weekly Schedule)
Mifumo ya Kutwa na Kambi (Physical Classes): Vipindi vinaendeshwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Kila siku kuna jumla ya vipindi vitatu (3) vya masomo tofauti kulingana na idara aliyosajiliwa mwanafunzi.
Mfumo wa Online (Virtual Classes): Masomo yanarushwa na kupatikana kupitia mfumo wetu wa kidijitali. Wanafunzi wanapokea mihadhara, video, na maelekezo ya moja kwa moja kila wiki, huku kukiwa na darasa maalum la mubashara (Live Session) kila mwisho wa wiki kwa ajili ya maswali na majibu.
B. Ratiba ya Kila Mwezi (Monthly Evaluation)
• Wiki ya 1 na ya 2: Ufundishaji wa kina wa mada mpya kulingana na vitabu vya ngazi husika.
• Wiki ya 3: Majaribio madogo ya vitendo na marudio ya mada zote zilizosomwa (Continuous Assessment).
• Wiki ya 4: Mitihani rasmi ya mwisho wa mwezi (Monthly Exams) kwa ajili ya kupima uelewa wa mwanafunzi na kutoa ripoti ya maendeleo.
C. Ratiba ya Mwaka (Academic Annual Calendar)
Mwaka wa masomo umegawanywa katika Mihula Miwili (Semesters 2) ya miezi sita sita:
- Muhula wa Kwanza (Januari – Juni): Ufunguzi wa masomo, kukamilisha nusu ya kwanza ya mtaala, na Mitihani ya Muhula wa Kwanza (Mid-Year Exams). Lipaswalo likifuatiwa na likizo fupi ya katikati ya mwaka.
- Muhula wa Pili (Julai – Desemba): Kukamilisha nusu ya pili ya mtaala, marudio makuu, Mitihani ya Mwisho wa Mwaka (Final Exams), na Mahafali ya kuhitimu ngazi husika.
3. Silabasi Kamili ya Masomo (Full Syllabus)
| Ngazi ya Masomo |
Muda wa Kusoma |
Mitaala na Vitabu Vinavyofundishwa |
Ngazi ya 1: TAMHIID (Msingi Mkuu / Utangulizi) |
Mwaka 1 (Semesters 2) |
1. Qur'an na Tajwiid: Al-Qaaidat Nnooraaniyyah, Tuhfatul Atwfaal.
2. Aqiidah: Thalaathatul Usool.
3. Fiqhi: Al-Fiqhul Muyassar.
4. Lugha ya Kiarabu: Duruus LLughatul Arabiyyah (Juzuu ya 1), Qawaaidul Imlaa.
5. Taariikh: Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 1).
|
Ngazi ya 2: MUTAWASSITWAH (Kati / Intermediate) |
Mwaka 1 (Semesters 2) |
1. Qur'an na Tajwiid: Hidaayatul Mustafiid.
2. Hadith: Al-Arba'iina Nnawawiyyah.
3. Fiqhi na Usuul: Matnul Ghaayat Wattaqriib (Abi Shujaa), Al-Waraqat.
4. Aqiidah: Al-Qawa'id Al-Arba', Kitab at-Tawheed.
5. Lugha ya Kiarabu: Al-Ajruumiyyah, Matnul Binaa wal-Asaas.
6. Taariikh: Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu ya 2 & 3).
7. Adyaan na Daawah: Kitaabul Kabaair, Adda'wah ila Llaah.
|
Ngazi ya 3: THAANAWIY (Juu / Advanced) |
Mwaka 1 (Semesters 2) |
1. Qur'an na Tajwiid: Matnul Jazariyyah.
2. Hadith: Umdatul Ahkaam, Buluughul Maraam.
3. Fiqhi: Manhaj Ssaalikiin.
4. Aqiidah: Al-Aqiidah Al-Waaswitwiyyah.
5. Taariikh na Siyrah: Ar-Raheequl Makhtoom, Qiswasul Anbiyaai.
6. Lugha ya Kiarabu: Al-Qiraa'at Rrashiidah.
7. Adyaan na Daawah: Al-Milal wa Nnihal.
|
4. Masharti na Taratibu za Masomo
- Ada ya kila kitengo hulipwa kwa mwezi mmoja kulingana na vitengo alivyochagua mwanafunzi.
- Ada inasaidia uendeshaji, majaribio ya kila siku, mitihani ya wiki na mitihani ya mwisho wa mwezi.
- Mwanafunzi anaruhusiwa kujionea mazingira na mfumo kwa wiki moja kabla ya kuanza kulipa ada.
- Mwanafunzi anaruhusiwa kuchagua kitengo kimoja au zaidi wakati wa usajili.
- Baada ya kuanza, hairuhusiwi kuongeza kitengo kipya mpaka kipindi cha vitengo vilivyosajiliwa kimalizike.
- Wanafunzi wa Kambi watapewa sehemu ya kulala (malazi) bila malipo, lakini wanatakiwa kuja na mahitaji binafsi (tandiko, nguo za heshima n.k).
- Wanafunzi wa Kambi watapatiwa kifungua kinywa nicotine chakula cha mchana bure. Chakula cha usiku kitakuwa jukumu lao.
- Wanafunzi wote wanapaswa kuzingatia maadili ya Kiislamu, nidhamu, usafi, na heshima kwa walimu.
Comments
Post a Comment
Karibu kutoa maoni yako. Tafadhali andika kwa heshima, maadili na lugha yenye kujenga jamii.