Maktaba ya Vitabu Na Nyaraka Rasmi
- Get link
- X
- Other Apps
MAKTABA YA VITABU NA NYARAKA RASMI
Ratiba ya Masomo: TAMHIID
Mchanganuo kamili wa vipindi vya kila wiki, muda wa masomo na mtiririko wa mihula miwili kwa wanafunzi wa Ngazi ya Kwanza (Tamhiid).
Ratiba ya Masomo: MUTAWASSITWAH
Ratiba rasmi ya darasani na mtandaoni kwa ajili ya wanafunzi wa Ngazi ya Kati (Mutawassitwah) wanaosoma mtaala wa mwaka mmoja.
Ratiba ya Masomo: THAANAWIY
Mwongozo wa masomo, vipindi na mihula miwili ya ufundishaji wa kina kwa wanafunzi wa Ngazi ya Juu (Thaanawiy).
Sheria na Kanuni za Mfumo wa Elimu AMAN VISSION
Nyaraka rasmi inayoeleza sheria za shule na vyuo vya Kiislamu, taratibu za ada, miongozo ya nidhamu kwa wanafunzi wa Kutwa (Day), Kambi (Bweni) na wale wa Mtandaoni (Online), pamoja na maadili ya jumla yanayopaswa kuzingatiwa wakati wote wa masomo.
Lengo Kuu: Hii ni ngazi ya msingi mkuu na utangulizi wa elimu ya Kiislamu. Inalenga kumjengea mwanafunzi uwezo thabiti wa kusoma Qur'ani kwa tajwiid sahihi tangu hatua ya herufi, kujua misingi ya itikadi (Aqiidah), kujifunza fikra sahihi za ibada za kila siku kama vile Twahara na Swala, na kuanza kupata msamiati wa Lugha ya Kiarabu pamoja na misingi ya uandishi (Imla).
Al-Qaaidat Nnooraaniyyah
Herufi na matamshi sahihi ya maneno ya Qur'an Tukufu.
Tuhfatul Atwfaal
Misingi ya Tajwiid ikiwemo sheria za Nun Sakina na Tanween.
Thalaathatul Usool
Misingi mitatu mikuu: Kumjua Mola wako, kumjua Mtume wako, na kuijua Dini yako.
Al-Fiqhul Muyassar
Misingi ya ibada za kila siku, ikizingatia sehemu ya Twahara na Swala.
Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu 1)
Historia ya maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W) katika kipindi cha Makka.
Duruus LLughatul Arabiyyah (Kitabu 1)
Misingi ya kwanza ya mazungumzo na herufi za Kiarabu.
Qawaaidul Imlaa
Misingi rahisi na ya mwanzoni ya uandishi na imla ya Kiarabu.
Lengo Kuu: Ngazi hii inamvusha mwanafunzi kutoka hatua ya awali kuelekea kiwango cha kati cha uchambuzi. Hapa mwanafunzi anasoma sheria za ndani zaidi za sarufi ya Kiarabu (Nahwu na Swarfu) ili kuanza kuelewa vitabu vya kielimu vilivyoandikwa kwa lugha asili. Pia masomo ya Fiqhi yanapanuka kupitia misingi ya kisheria (Al-Usuul), na masomo ya Tauhidi yanajikita katika kulinda na kuelewa vyema mipaka ya imani.
Hidaayatul Mustafiid
Sheria kamili za Tajwiid zilizopangwa kwa mfumo wa maswali na majibu.
Al-Arba'iina Nnawawiyyah
Misingi mikuu na miongozo ya dini kupitia hadithi arobaini za Imam An-Nawawi.
Matnul Ghaayat Wattaqriib
Kitabu cha Abi Shujaa'h kinachofundisha Fiqhi ya kina ya ibada na muamalat.
Al-Waraqat
Kitabu mashuhuri cha Imam Al-Juwayni kinachotoa utangulizi wa misingi ya Fiqhi.
Al-Qawa'id Al-Arba'
Kanuni nne muhimu katika kuelewa na kujiepusha na shirki (ushirikina).
Kitab at-Tawheed
Ufafanuzi wa kina na thabiti kuhusu Tauhidi ya ibada pekee kwa Allah.
Khulaaswat Nnuurul Yaqiin (Juzuu 2 & 3)
Historia ya Mtume (S.A.W) kipindi cha Madina pamoja na historia ya Khilafa.
Al-Ajruumiyyah
Kitabu kikuu cha misingi ya sarufi ya lugha ya Kiarabu (Nahwu).
Matnul Binaa wal-Asaas
Kitabu kinachofundisha mfumo na mnyambuliko wa maneno ya Kiarabu (Swarfu).
Kitaabul Kabaair
Kitabu kinachofundisha madambi makubwa ili mwislamu aweze kujiepusha nayo.
Adda'wah ila Llaah
Mbinu, hekima na busara za mwanzo za ulinganizi na uenezaji wa heri.
Lengo Kuu: Hiki ni kiwango cha juu cha Maandalizi ya Kida'wah na Uongozi wa Kijamii. Wanafunzi wanajikita kwenye vitabu vikubwa vya Hadithi zenye hukumu (Ahkam), kuelewa kwa mapana masuala ya Aqiidah ya Ahlus Sunnah, kusoma historia za kina za mitume na wasifu wa Mtume (Siirah), pamoja na kupata ujuzi thabiti wa usemi, uandishi wa juu wa Kiarabu, kulinganisha dini, na mbinu za kiungozi katika jamii.
Matnul Jazariyyah
Kitabu cha ushairi kinachofafanua kwa kina sifa na matamshi sahihi ya herufi za Qur'an.
Umdatul Ahkaam
Mkusanyiko wa hadithi za kisheria (Ahkam) zilizochukuliwa kutoka vyanzo sahihi kabisa.
Buluughul Maraam
Kitabu cha hadithi kilichopangwa kwa kufuata milango ya kisheria na kifiqhi.
Manhaj Ssaalikiin
Ufafanuzi wa Fiqhi ya kielimu na kivitendo isiyofungamana na upande wa madhehebu.
Al-Aqiidah Al-Waaswitwiyyah
Itikadi sahihi ya Ahlus Sunnah wal Jama'ah juu ya Majina na Sifa tukufu za Allah.
Ar-Raheequl Makhtoom
Kitabu kinachotoa wasifu na historia ya kina kabisa ya maisha ya Mtume (S.A.W).
Qiswasul Anbiyaai
Historia na kisa cha kuvutia cha Mitume waliotangulia kilichoandikwa na Ibn Kathiir.
Al-Qiraa'at Rrashiidah
Kukuza uwezo wa kusoma, kupata msamiati, matumizi ya usemi na uandishi wa juu.
Al-Milal wa Nnihal
Kitabu kinachofundisha kuelewa makundi, madhehebu, na kulinganisha dini nyingine.
Comments
Post a Comment
Karibu kutoa maoni yako. Tafadhali andika kwa heshima, maadili na lugha yenye kujenga jamii.